Proverbs 21


1 aMoyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana;
huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo.


2 bNjia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake,
bali Bwana huupima moyo.


3 cKufanya yaliyo sawa na haki inakubalika
zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.


4 dMacho ya kudharau na moyo wa kiburi,
ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!


5 eMipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida,
kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.


6 fMali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo
ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.


7 gJeuri ya waovu itawaburuta mbali,
kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa.


8 hNjia ya mwenye hatia ni ya upotovu,
bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu.


9 iNi afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba,
kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.


10 jMtu mwovu hutamani sana ubaya,
jirani yake hapati huruma kutoka kwake.


11 kWakati mwenye mzaha ameadhibiwa,
mjinga hupata hekima;
wakati mtu mwenye hekima afundishwapo,
hupata maarifa.


12 lMwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu,
naye atawaangamiza waovu.


13 mMtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini,
yeye pia atalia, wala hatajibiwa.


14 nZawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira
na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali.


15 oWakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki,
bali kitisho kwa watenda mabaya.


16 pMtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu,
hupumzika katika kundi la waliokufa.


17 qMtu apendaye anasa atakuwa maskini,
yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri.


18 rWaovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki,
nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu.


19 sNi afadhali kuishi jangwani
kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.


20 tKatika nyumba ya mwenye hekima
kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta,
lakini mtu mpumbavu
hutafuna vyote alivyo navyo.


21 uYeye afuatiaye haki na upendo
hupata uzima, mafanikio na heshima.


22 vMtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu,
na kuangusha ngome wanazozitegemea.


23 wYeye alindaye kinywa chake na ulimi wake
hujilinda na maafa.


24 xMtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake;
hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.


25 yKutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake,
kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.


26 zMchana kutwa hutamani zaidi,
lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.


27 aaDhabihu ya mtu mwovu ni chukizo,
si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya!


28 abShahidi wa uongo ataangamia,
bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu.


29 acMtu mwovu ana uso wa ushupavu,
bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake.


30 adHakuna hekima, wala akili, wala mpango
unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.


31 aeFarasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita,
bali ushindi huwa kwa Bwana.
Copyright information for SwhKC